Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mke wa mwana wako, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
1 Samueli 14:44 - Swahili Revised Union Version Naye Sauli akasema, Mungu anifanyie hivi, na kuzidi; kwa kuwa hakika utakufa, Yonathani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shauli akasema, “Mungu na anitendee mimi vivyo hivyo na hata na wengine. Yonathani ni lazima utauawa.” Biblia Habari Njema - BHND Shauli akasema, “Mungu na anitendee mimi vivyo hivyo na hata na wengine. Yonathani ni lazima utauawa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shauli akasema, “Mungu na anitendee mimi vivyo hivyo na hata na wengine. Yonathani ni lazima utauawa.” Neno: Bibilia Takatifu Sauli akasema, “Mungu na aniadhibu vikali zaidi kama wewe Yonathani hutakufa.” Neno: Maandiko Matakatifu Sauli akasema, “Mungu na anishughulikie kwa ukali zaidi kama wewe Yonathani hutakufa.” BIBLIA KISWAHILI Naye Sauli akasema, Mungu anifanyie hivi, na kuzidi; kwa kuwa hakika utakufa, Yonathani. |
Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mke wa mwana wako, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.
Ndipo hasira ya Daudi ikawaka sana juu ya mtu yule; akamwambia Nathani, Aishivyo BWANA, mtu huyo aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa;
Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
Mungu amfanyie Abneri vivyo hivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile BWANA alivyomwapia;
Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.
Pale utakapofia ndipo nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
Kwa maana, kama aishivyo BWANA, awaokoaye Waisraeli, hata ikiwa iko kwa Yonathani, mwanangu, hakika atakufa. Lakini miongoni mwa watu wote hakuna mtu yeyote aliyemjibu.
Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mmoja wa kiume, kutakapopambazuka.
Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Mungu akufanyie vivyo hivyo, na kuzidi, ukinificha lolote katika hayo yote BWANA aliyosema nawe.