Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 3:9 - Swahili Revised Union Version

9 Mungu amfanyie Abneri vivyo hivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile BWANA alivyomwapia;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mungu aniue ikiwa sitatekeleza yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mungu aniue ikiwa sitatekeleza yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mungu aniue ikiwa sitatekeleza yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mungu na amwadhibu Abneri vikali zaidi ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile Mwenyezi Mungu alichomwahidi kwa kiapo,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Mungu na amshughulikie Abneri, tena kwa ukali, ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile bwana alichomwahidi kwa kiapo,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Mungu amfanyie Abneri vivyo hivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile BWANA alivyomwapia;

Tazama sura Nakili




2 Samueli 3:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.


Akawainamisha mioyo watu wote wa Yuda, kama mtu mmoja; basi wakatuma kwa mfalme, Rudi wewe na watumishi wako wote.


Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, kukiwa bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo hivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine chochote kabla ya jua kutua.


Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.


Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe.


Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumpa ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la BWANA.


Pale utakapofia ndipo nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.


Naye Sauli akasema, Mungu anifanyie hivi, na kuzidi; kwa kuwa hakika utakufa, Yonathani.


Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.


Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mmoja wa kiume, kutakapopambazuka.


Yeye BWANA amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; BWANA amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.


Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Mungu akufanyie vivyo hivyo, na kuzidi, ukinificha lolote katika hayo yote BWANA aliyosema nawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo