Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zekaria 6:3 - Swahili Revised Union Version

na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

la tatu lilikokotwa na farasi weupe, na la nne lilikokotwa na farasi wa kijivujivu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

la tatu lilikokotwa na farasi weupe, na la nne lilikokotwa na farasi wa kijivujivu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

la tatu lilikokotwa na farasi weupe, na la nne lilikokotwa na farasi wa kijivujivu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

la tatu lilivutwa na farasi weupe, na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zekaria 6:3
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, niliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka.


miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.


Niliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya miti ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe.


Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.


Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.


Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, huku akishinda tena apate kushinda.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa wanyama wa nchi.