Zaburi 102:8 - Swahili Revised Union Version Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Wakitaja jina langu katika laana zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchana kutwa maadui zangu wananisimanga, wanaonidhihaki hutumia jina langu kulaania. Biblia Habari Njema - BHND Mchana kutwa maadui zangu wananisimanga, wanaonidhihaki hutumia jina langu kulaania. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchana kutwa maadui zangu wananisimanga, wanaonidhihaki hutumia jina langu kulaania. Neno: Bibilia Takatifu Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki; wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana. Neno: Maandiko Matakatifu Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki, wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana. BIBLIA KISWAHILI Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Wakitaja jina langu katika laana zao. |
Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine.
Tena kwa ajili yao laana itatumiwa na wafungwa wote wa Yuda, walioko Babeli, kusema, BWANA akufanye uwe kama Sedekia, na kama Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka motoni;
Na mara nyingi katika masinagogi yote niliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama mwenye wazimu, nikawaudhi hata katika miji ya ugenini.
Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Matusi yao waliokutusi wewe yalinipata mimi.