Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni, Hamkuu wa wakuu wa majeshi; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.
Yoshua 23:10 - Swahili Revised Union Version Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu wenu mmoja tu anaweza kuwakimbiza maadui elfu, kwani Mwenyezi-Mungu Mungu wenu ndiye anayewapigania kama alivyowaahidi. Biblia Habari Njema - BHND Mtu wenu mmoja tu anaweza kuwakimbiza maadui elfu, kwani Mwenyezi-Mungu Mungu wenu ndiye anayewapigania kama alivyowaahidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu wenu mmoja tu anaweza kuwakimbiza maadui elfu, kwani Mwenyezi-Mungu Mungu wenu ndiye anayewapigania kama alivyowaahidi. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapigania, kama alivyoahidi. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapigania, kama alivyoahidi. BIBLIA KISWAHILI Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia. |
Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni, Hamkuu wa wakuu wa majeshi; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.
Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.
Kwani walianguka wengi waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa katika nchi yao hadi wakati wa ule uhamisho.
Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia moja, na watu mia moja wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao.
awaambie, Sikilizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao;
kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Akasema, Nitawaficha uso wangu, Nitaona mwisho wao utakuwaje; Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, Watoto wasio imani ndani yao.
Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa?
Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli,
nanyi mmeona mambo yote ambayo BWANA, Mungu wenu, amewatenda mataifa haya yote kwa ajili yenu; kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye aliyewapigania ninyi.
Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akaua watu elfu moja kwa mfupa huo;
Tena baada ya Ehudi alikuwapo Shamgari mwana wa Anathi, aliyewaua Wafilisti watu mia sita kwa fimbo ya kuswagia ng'ombe; naye aliwaokoa Israeli.
Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na twende tukavuke ngomeni mwa hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kama ni kwa wengi au kama ni kwa wachache.