Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yoyote.
Yoshua 21:2 - Swahili Revised Union Version wakanena nao hapo Shilo katika nchi ya Kanaani, wakisema, Yeye BWANA aliamuru kwa mkono wa Musa kwamba sisi tupewe miji tupate kukaa humo, mbuga zake za malisho kwa ajili ya mifugo wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wakawaambia, “Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose tupewe miji ya kuishi na mbuga za malisho ya wanyama wetu.” Biblia Habari Njema - BHND wakawaambia, “Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose tupewe miji ya kuishi na mbuga za malisho ya wanyama wetu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wakawaambia, “Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose tupewe miji ya kuishi na mbuga za malisho ya wanyama wetu.” Neno: Bibilia Takatifu huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Mwenyezi Mungu aliamuru kupitia Musa kuwa mtupe miji ya kuishi yenye maeneo ya malisho kwa mifugo yetu.” Neno: Maandiko Matakatifu huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “bwana aliamuru kupitia Musa kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa mifugo yetu.” BIBLIA KISWAHILI wakanena nao hapo Shilo katika nchi ya Kanaani, wakisema, Yeye BWANA aliamuru kwa mkono wa Musa kwamba sisi tupewe miji tupate kukaa humo, mbuga zake za malisho kwa ajili ya mifugo yetu. |
Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yoyote.
wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mfanyakazi astahili posho yake.
Vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa, hao wana wa Israeli walifanya hivyo, nao wakaigawanya hiyo nchi.
Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.
Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na mbuga zake za malisho, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya BWANA.