Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 21:1 - Swahili Revised Union Version

1 Wakati huo hao vichwa vya nyumba za mababa ya Walawi wakamwendea kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni na viongozi wa hao waliokuwa viongozi wa familia za makabila ya Waisraeli;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Walipokuwa huko Shilo katika nchi ya Kanaani viongozi wa koo za Walawi wakawaendea kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa za makabila yote ya Waisraeli,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Walipokuwa huko Shilo katika nchi ya Kanaani viongozi wa koo za Walawi wakawaendea kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa za makabila yote ya Waisraeli,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Walipokuwa huko Shilo katika nchi ya Kanaani viongozi wa koo za Walawi wakawaendea kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa za makabila yote ya Waisraeli,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Wakati huo hao vichwa vya nyumba za mababa wa Walawi wakamwendea kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni na viongozi wa hao waliokuwa viongozi wa familia za makabila ya Waisraeli;

Tazama sura Nakili

Yoshua 21:1
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.

Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni.

Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba wa Walawi kulingana na jamaa zao.

Kisha BWANA akanena na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko, akamwambia,

Tena katika miji mtakayotoa ya hiyo milki ya wana wa Israeli, katika hao walio wengi mtatwaa miji mingi; na katika hao walio wachache mtatwaa miji michache; kila mtu kama ulivyo urithi wake atakaourithi, atawapa Walawi katika miji yake.

Kisha hizi ndizo nchi ambazo wana wa Israeli walizitwaa katika nchi ya Kanaani, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na vichwa vya nyumba za mababa wa makabila ya Israeli, waliwagawanyia,

Nao wakaja mbele ya kuhani Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya viongozi, wakasema, BWANA alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuifuata hiyo amri ya BWANA akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.

Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo