Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
Yoshua 18:8 - Swahili Revised Union Version Basi watu hao wakainuka wakaenda; Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuichunguza nchi, akawaambia, Nendeni, mkapite katikati ya nchi, na kuandika habari zake, kisha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za BWANA huko Shilo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza nchi. Kabla hawajaenda, Yoshua akawapa maagizo: “Nendeni nchini kote mkaandike maelezo kamili juu ya hiyo nchi, kisha mrudi mnieleze, nami nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu hapa hapa Shilo kuhusu sehemu mtakayopewa.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza nchi. Kabla hawajaenda, Yoshua akawapa maagizo: “Nendeni nchini kote mkaandike maelezo kamili juu ya hiyo nchi, kisha mrudi mnieleze, nami nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu hapa hapa Shilo kuhusu sehemu mtakayopewa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, watu hao wakaanza safari ya kwenda kuichunguza nchi. Kabla hawajaenda, Yoshua akawapa maagizo: “Nendeni nchini kote mkaandike maelezo kamili juu ya hiyo nchi, kisha mrudi mnieleze, nami nitapiga kura mbele ya Mwenyezi-Mungu hapa hapa Shilo kuhusu sehemu mtakayopewa.” Neno: Bibilia Takatifu Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuikagua hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo yake. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za Mwenyezi Mungu.” Neno: Maandiko Matakatifu Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo kuihusu. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za bwana.” BIBLIA KISWAHILI Basi watu hao wakainuka wakaenda; Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuichunguza nchi, akawaambia, Nendeni, mkapite katikati ya nchi, na kuandika habari zake, kisha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za BWANA huko Shilo. |
Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi.
Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila tisa, na nusu ya kabila la Manase.
Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.
Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.
Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.
Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele ya BWANA, Mungu wetu.
Basi watu hao wakaenda, wakapita katikati ya nchi, wakaandika habari zake katika kitabu, na kuigawanya kwa miji yake, hata iwe mafungu saba, kisha wakamrejea Yoshua kambini huko Shilo.
Kwa hiyo Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, [Kwa nini usimjibu mtumishi wako leo? Ikiwa dhambi iko ndani yangu, au ndani yake Yonathani mwanangu, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi iko katika watu wako Israeli,] utoe Thumimu. Basi Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu wakapona.