Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 18:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini Walawi hawatapata sehemu yoyote kati yenu, maana sehemu yao ni kuwa makuhani wa kumhudumia Mwenyezi-Mungu. Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase walikwisha pata sehemu yao upande wa mashariki wa mto Yordani. Walipewa sehemu hii na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini Walawi hawatapata sehemu yoyote kati yenu, maana sehemu yao ni kuwa makuhani wa kumhudumia Mwenyezi-Mungu. Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase walikwisha pata sehemu yao upande wa mashariki wa mto Yordani. Walipewa sehemu hii na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa Mwenyezi Mungu ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa bwana ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Musa mtumishi wa bwana aliwapa.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.

Tazama sura Nakili

Yoshua 18:7
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha BWANA akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lolote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli.

Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi.

Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.

Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; BWANA ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia BWANA, Mungu wako.)

Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase iwe urithi wao.

Lakini Musa hakuwapa kabila la Lawi urithi uwao wote; yeye BWANA, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo