Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja.
Yoshua 17:8 - Swahili Revised Union Version Hiyo nchi ya Tapua ilikuwa ni mali ya Manase; lakini ule mji wa Tapua uliokuwa katika mpaka wa Manase ulikuwa ni mali ya wana wa Efraimu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nchi ya Tapua ilikuwa mali yake Manase, lakini mji wa Tapua, ambao ulikuwa mpakani, ulikuwa mali ya wazawa wa Efraimu. Biblia Habari Njema - BHND Nchi ya Tapua ilikuwa mali yake Manase, lakini mji wa Tapua, ambao ulikuwa mpakani, ulikuwa mali ya wazawa wa Efraimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nchi ya Tapua ilikuwa mali yake Manase, lakini mji wa Tapua, ambao ulikuwa mpakani, ulikuwa mali ya wazawa wa Efraimu. Neno: Bibilia Takatifu (Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.) Neno: Maandiko Matakatifu (Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.) BIBLIA KISWAHILI Hiyo nchi ya Tapua ilikuwa ni mali ya Manase; lakini ule mji wa Tapua uliokuwa katika mpaka wa Manase ulikuwa ni mali ya wana wa Efraimu. |
Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja.
Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hadi kijito cha Kana; na mwisho wake ulikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao;
Mpaka wa Manase ulikuwa kutoka Asheri hadi Mikmeta, ulioelekea Shekemu; tena mpaka ukaendelea upande wa kulia, hata kuwafikia wenyeji wa Entapua.