Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 16:8 - Swahili Revised Union Version

8 Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hadi kijito cha Kana; na mwisho wake ulikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kutoka Tapua, mpaka ulienda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, kufuatana na koo zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hadi kijito cha Kana; na mwisho wake ulikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao;

Tazama sura Nakili

Yoshua 16:8
10 Marejeleo ya Msalaba  

akamweka awe mfalme wa Gileadi, na Waasheri, na Yezreeli, na Efraimu, na Benyamini, na juu ya Israeli wote.

Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja.

Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; huu ndio mpaka wenu upande wa magharibi.

mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja;

pamoja na ile miji iliyotengwa kwa ajili ya wana wa Efraimu katikati ya urithi wa hao wana wa Manase, miji yote pamoja na vijiji vyake.

Mpaka wa Manase ulikuwa kutoka Asheri hadi Mikmeta, ulioelekea Shekemu; tena mpaka ukaendelea upande wa kulia, hata kuwafikia wenyeji wa Entapua.

na Ebroni, Rehobu, Hamoni, Kana, hadi kufikia Sidoni Kuu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo