Wakavuka Yordani, wakapiga kambi huko Aroeri, upande wa kulia wa mji ulioko kati ya bonde la Gadi, na mpaka Yazeri;
Yoshua 13:16 - Swahili Revised Union Version Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ilikuwa kuanzia Aroeri kando ya bonde la Arnoni na mji uliokuwa katika bonde hilo pamoja na nchi yote ya tambarare ya Medeba. Biblia Habari Njema - BHND ilikuwa kuanzia Aroeri kando ya bonde la Arnoni na mji uliokuwa katika bonde hilo pamoja na nchi yote ya tambarare ya Medeba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ilikuwa kuanzia Aroeri kando ya bonde la Arnoni na mji uliokuwa katika bonde hilo pamoja na nchi yote ya tambarare ya Medeba. Neno: Bibilia Takatifu Eneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba Neno: Maandiko Matakatifu Eneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba BIBLIA KISWAHILI Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba; |
Wakavuka Yordani, wakapiga kambi huko Aroeri, upande wa kulia wa mji ulioko kati ya bonde la Gadi, na mpaka Yazeri;
Basi wakakodi magari elfu thelathini na mbili, na mfalme wa Maaka na watu wake; nao walikuja wakatua mbele ya Medeba. Na wana wa Amoni wakakusanyika kutoka miji yao, wakaja vitani.
Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.
Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.
Na nchi hiyo tuliitwaa ikawa milki yetu, wakati huo; kutoka Aroeri iliyo kwenye bonde la Arnoni, na nusu ya nchi ya milima ya Gileadi, na miji iliyokuwamo, niliwapa Wareubeni na Wagadi;
Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hadi kuufikia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni;
kutoka huko Aroeri, iliyoko pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulioko pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni;
Kwa kuwa Musa alikuwa amekwisha kuwapa urithi hayo makabila mawili na nusu, ng'ambo ya pili ya Yordani; lakini hakuwapa Walawi urithi wowote kati yao.
Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.
Wakati Israeli walipokuwa wakikaa Heshboni na miji yake, na katika Aroeri na miji yake, na katika miji hiyo yote iliyo huko kando ya Arnoni, muda wa miaka mia tatu; mbona hamkuikomboa wakati huo?