Yoshua 10:16 - Swahili Revised Union Version Na hawa wafalme watano wakakimbia, wakajificha ndani ya pango la Makeda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wafalme watano walikimbia na kujificha katika pango la Makeda. Biblia Habari Njema - BHND Wale wafalme watano walikimbia na kujificha katika pango la Makeda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wafalme watano walikimbia na kujificha katika pango la Makeda. Neno: Bibilia Takatifu Basi wale wafalme watano wakawa wamekimbia kujificha kwenye pango huko Makeda. Neno: Maandiko Matakatifu Basi wale wafalme watano wakawa wamekimbia kujificha kwenye pango huko Makeda. BIBLIA KISWAHILI Na hawa wafalme watano wakakimbia, wakajificha ndani ya pango la Makeda. |
Kwa nini kulala mazizini arukapo hua, Mbawa zake ziking'aa kama fedha Na manyoya yake kama dhahabu?
Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko.
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.
Kisha Yoshua aliambiwa habari hiyo, ya kwamba, Hao wafalme watano wameonekana, nao wamejificha ndani ya pango ya Makeda
Ndipo hao wafalme watano wa Waamori, mfalme wa Yerusalemu, na mfalme wa Hebroni na mfalme wa Yarmuthi na mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Egloni, wakakutana pamoja, kisha wakakwea, wao na majeshi yao yote, na kupiga kambi yao kinyume cha Gibeoni, na kuupiga vita.
Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na muungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
Mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome.
Hata Waisraeli walipoona ya kuwa wako katika dhiki, (maana watu walifadhaishwa), ndipo hao watu wakajificha katika mapango, na katika vichaka, na katika miamba, na katika mashimo, na katika mabirika.
Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kwenda haja. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana.
Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hadi chini, akamsujudia.