Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao.
Yona 2:8 - Swahili Revised Union Version Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili, huutupilia mbali uaminifu wao kwako. Biblia Habari Njema - BHND Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili, huutupilia mbali uaminifu wao kwako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili, huutupilia mbali uaminifu wao kwako. Neno: Bibilia Takatifu “Wale watu wanaoshikilia sanamu batili hupoteza neema yao. Neno: Maandiko Matakatifu “Wale watu wanaong’ang’ana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao. BIBLIA KISWAHILI Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe. |
Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao.
Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.
Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe kutoka kwa wanaonichukia, Na kutoka katika vilindi vya maji.
Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.
Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.
Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.