Yona 2:6 - Swahili Revised Union Version Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni. Biblia Habari Njema - BHND Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni. Neno: Bibilia Takatifu Nilizama chini sana hata pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu. BIBLIA KISWAHILI Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu, |
Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.
Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako?
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.
Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiria mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?
ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.
ili mti wowote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.
Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.
Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.