Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 38:17 - Swahili Revised Union Version

17 Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Nilipata mateso makali kwa faida yangu; lakini umeyaokoa maisha yangu kutoka shimo la uharibifu, maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Nilipata mateso makali kwa faida yangu; lakini umeyaokoa maisha yangu kutoka shimo la uharibifu, maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Nilipata mateso makali kwa faida yangu; lakini umeyaokoa maisha yangu kutoka shimo la uharibifu, maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Hakika ilikuwa ya faida yangu ndiyo maana nikapata maumivu makali. Katika upendo wako ukaniokoa kutoka shimo la uharibifu; umeziweka dhambi zangu zote nyuma yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Hakika ilikuwa ya faida yangu ndiyo maana nikapata maumivu makali. Katika upendo wako ukaniokoa kutoka shimo la uharibifu; umeziweka dhambi zangu zote nyuma yako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

Tazama sura Nakili




Isaya 38:17
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kiota changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;


Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi.


Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.


Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.


Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,


Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi, Akutia taji la fadhili na rehema,


Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.


Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.


Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.


Umeusamehe uovu wa watu wako, Umezisitiri hatia zao zote.


Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.


Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.


Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.


Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,


Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nilimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakufikia, Katika hekalu lako takatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo