Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakashindwa kuupata mlango.
Yohana 8:59 - Swahili Revised Union Version Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. Biblia Habari Njema - BHND Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Isa akajificha, naye akatoka Hekaluni. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Isa akajificha, naye akatoka Hekaluni. BIBLIA KISWAHILI Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni. |
Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakashindwa kuupata mlango.
Na yeyote atakayelaani jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzaliwa, hapo atakapolaani jina la BWANA atauawa.
Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone.
Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu.
Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.