Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?
Yohana 8:51 - Swahili Revised Union Version Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.” Biblia Habari Njema - BHND Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.” Neno: Bibilia Takatifu Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu, hataona mauti milele.” Neno: Maandiko Matakatifu Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu hataona mauti milele.” BIBLIA KISWAHILI Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. |
Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?
Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.
Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma ana uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nilishika.
Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo kwa muda kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.