Mfalme asema hivi, Hezekia asiwadanganye; kwa maana, hataweza kuwaokoa katika mkono wake.
Yohana 7:47 - Swahili Revised Union Version Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mafarisayo wakawauliza, “Je, nanyi pia mmedanganyika? Biblia Habari Njema - BHND Mafarisayo wakawauliza, “Je, nanyi pia mmedanganyika? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mafarisayo wakawauliza, “Je, nanyi pia mmedanganyika? Neno: Bibilia Takatifu Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika? Neno: Maandiko Matakatifu Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika? BIBLIA KISWAHILI Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? |
Mfalme asema hivi, Hezekia asiwadanganye; kwa maana, hataweza kuwaokoa katika mkono wake.
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, BWANA atatuokoa.
Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lolote, wala wa ufalme wowote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu?
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huivunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa angali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.
Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.
kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli;