Yohana 6:69 - Swahili Revised Union Version Nasi tumeamini, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu” Biblia Habari Njema - BHND Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu” Neno: Bibilia Takatifu Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.” Neno: Maandiko Matakatifu Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.” BIBLIA KISWAHILI Nasi tumeamini, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu. |
Naye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo.
Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu.
Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nilisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.
Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [
hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.