Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Yohana 6:3 - Swahili Revised Union Version Naye Yesu akapanda mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. Biblia Habari Njema - BHND Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Isa akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Isa akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. BIBLIA KISWAHILI Naye Yesu akapanda mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. |
Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.
Naye alipowaona makundi ya watu, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;
Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba.
Kisha Yesu, alipotambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.