Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
Yohana 4:3 - Swahili Revised Union Version aliondoka Yudea, akaenda zake tena mpaka Galilaya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya; Biblia Habari Njema - BHND Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya; Neno: Bibilia Takatifu Bwana Isa alipojua mambo haya, aliondoka Yudea akarudi tena Galilaya. Neno: Maandiko Matakatifu Bwana Isa alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya. BIBLIA KISWAHILI aliondoka Yudea, akaenda zake tena mpaka Galilaya. |
Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
Naye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Yudea,
Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.
Kesho yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.
Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka katika nchi ya Yudea; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.
Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.
Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yudea mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa karibu kufa.
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua.