Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
Yohana 1:37 - Swahili Revised Union Version Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao wanafunzi walimsikia Yohane akisema maneno hayo, wakamfuata Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Hao wanafunzi walimsikia Yohane akisema maneno hayo, wakamfuata Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao wanafunzi walimsikia Yohane akisema maneno hayo, wakamfuata Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yahya akisema haya, wakamfuata Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yahya akisema haya, wakamfuata Isa. BIBLIA KISWAHILI Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. |
Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za BWANA, na kumtafuta BWANA wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.
Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
Kesho yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.
Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.