Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Zekaria 8:21 - Swahili Revised Union Version

21 wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za BWANA, na kumtafuta BWANA wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Wakazi wa mji mmoja watawaendea wakazi wa mji mwingine na kuwaambia, ‘Twendeni pamoja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kumwomba baraka!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Wakazi wa mji mmoja watawaendea wakazi wa mji mwingine na kuwaambia, ‘Twendeni pamoja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kumwomba baraka!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Wakazi wa mji mmoja watawaendea wakazi wa mji mwingine na kuwaambia, ‘Twendeni pamoja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kumwomba baraka!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 na wenyeji wa mji mmoja wataenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi Mwenyezi Mungu, na kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Mimi mwenyewe ninaenda.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi bwana, na kumtafuta bwana Mwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za BWANA, na kumtafuta BWANA wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.

Tazama sura Nakili

Zekaria 8:21
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao.

Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.

Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa BWANA, Mungu wetu.

Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.

Basi watu wa Betheli walikuwa wamewatuma Shareza na Regem-meleki, na watu wao, ili kuomba fadhili za BWANA,

Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA wa majeshi, na kuomba fadhili za BWANA.

Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo