Yoeli 3:14 - Swahili Revised Union Version Umati mkubwa, umati mkubwa, wamo katika bonde la kukata kauli! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata kauli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanafika makundi kwa makundi kwenye bonde la Hukumu, maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia. Biblia Habari Njema - BHND Wanafika makundi kwa makundi kwenye bonde la Hukumu, maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanafika makundi kwa makundi kwenye bonde la Hukumu, maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia. Neno: Bibilia Takatifu Umati mkubwa, umati mkubwa katika bonde la uamuzi! Kwa kuwa siku ya Mwenyezi Mungu ni karibu katika bonde la uamuzi. Neno: Maandiko Matakatifu Umati mkubwa, umati mkubwa katika bonde la uamuzi! Kwa kuwa siku ya bwana ni karibu katika bonde la uamuzi. BIBLIA KISWAHILI Umati mkubwa, umati mkubwa, wamo katika bonde la kukata kauli! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata kauli. |
Kelele milimani kama kelele za watu wengi sana; kelele za falme za mataifa waliokutana pamoja; BWANA wa majeshi anapanga jeshi kwa vita;
Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya madari ya nyumba?
Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;
naye BWANA anatoa sauti yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?
Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.
nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.
Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.