Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoeli 3:12 - Swahili Revised Union Version

12 Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Haya mataifa na yajiweke tayari; yaje kwenye bonde liitwalo: ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’. Huko, mimi Mwenyezi-Mungu, nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Haya mataifa na yajiweke tayari; yaje kwenye bonde liitwalo: ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’. Huko, mimi Mwenyezi-Mungu, nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Haya mataifa na yajiweke tayari; yaje kwenye bonde liitwalo: ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’. Huko, mimi Mwenyezi-Mungu, nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyo kila upande.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.

Tazama sura Nakili




Yoeli 3:12
17 Marejeleo ya Msalaba  

Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipomtukuza BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.


BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.


Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.


Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.


Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.


Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya madari ya nyumba?


BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.


Kwa maana siku ile i karibu, siku ile ya BWANA i karibu, siku ya mawingu; itakuwa wakati wa maangamizi kwa mataifa.


Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.


Umati mkubwa, umati mkubwa, wamo katika bonde la kukata kauli! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata kauli.


nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.


Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.


Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.


Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo