Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoeli 1:15 - Swahili Revised Union Version

15 Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Ole wetu kwa ile siku ya Mwenyezi-Mungu, siku hiyo ya Mwenyezi-Mungu inakaribia; inakuja pamoja na maangamizi, kutoka kwa Mungu Mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Ole wetu kwa ile siku ya Mwenyezi-Mungu, siku hiyo ya Mwenyezi-Mungu inakaribia; inakuja pamoja na maangamizi, kutoka kwa Mungu Mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Ole wetu kwa ile siku ya Mwenyezi-Mungu, siku hiyo ya Mwenyezi-Mungu inakaribia; inakuja pamoja na maangamizi, kutoka kwa Mungu Mkuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Ole kwa siku hiyo! Kwa kuwa siku ya Mwenyezi Mungu iko karibu; itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ole kwa siku hiyo! Kwa kuwa siku ya bwana iko karibu; itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.

Tazama sura Nakili




Yoeli 1:15
18 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.


Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa kutoka kwayo.


Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.


Kwa maana siku ile i karibu, siku ile ya BWANA i karibu, siku ya mawingu; itakuwa wakati wa maangamizi kwa mataifa.


naye BWANA anatoa sauti yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?


Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.


Umati mkubwa, umati mkubwa, wamo katika bonde la kukata kauli! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata kauli.


Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.


Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya BWANA iko karibu; Kwa kuwa BWANA ametayarisha dhabihu, Amewatakasa wageni wake.


Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kuistahimili?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo