Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoeli 1:14 - Swahili Revised Union Version

14 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Waiteni wazee na wote wanaoishi katika nchi waende katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, wakamlilie Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Iteni wazee na wote waishio katika nchi waende katika nyumba ya bwana Mwenyezi Mungu wenu, wakamlilie bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,

Tazama sura Nakili




Yoeli 1:14
15 Marejeleo ya Msalaba  

Yehu akasema, Takaseni kusanyiko la dini kwa Baali. Wakalitangaza.


Wakasimama Yuda wote mbele za BWANA, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.


Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hadi siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha Torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa.


Nenda ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Susa, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.


Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea; Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.


Basi, ikawa katika mwaka wa tano wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa tisa, watu wote waliokuwa katika Yerusalemu, na watu wote waliokuja Yerusalemu kutoka miji yote ya Yuda, wakapiga mbiu ya kufunga mbele za BWANA.


Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu?


Mtamsogezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamtolea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.


Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, kuanzia yeye aliye mkubwa hadi aliye mdogo.


bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake.


Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo