Yoeli 1:8 - Swahili Revised Union Version Omboleza kama mwanamwali avaaye magunia Kwa ajili ya mume wa ujana wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lieni kama msichana aliyevaa vazi la gunia akiombolezea kifo cha mchumba wake. Biblia Habari Njema - BHND Lieni kama msichana aliyevaa vazi la gunia akiombolezea kifo cha mchumba wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lieni kama msichana aliyevaa vazi la gunia akiombolezea kifo cha mchumba wake. Neno: Bibilia Takatifu Omboleza kama bikira aliyevaa gunia akimwomboleza mume wa ujana wake. Neno: Maandiko Matakatifu Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake. BIBLIA KISWAHILI Omboleza kama mwanamwali avaaye magunia Kwa ajili ya mume wa ujana wake. |
Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;
Tetemekeni, enyi wanawake mnaostarehe; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu; jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, na kujivika nguo za magunia viunoni.
Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu.
Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzawa mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.