Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Yoeli 1:18 - Swahili Revised Union Version Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama wanyama wanavyolia kwa huzuni! Makundi ya ng'ombe yanahangaika, kwa sababu yamekosa malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka. Biblia Habari Njema - BHND Tazama wanyama wanavyolia kwa huzuni! Makundi ya ng'ombe yanahangaika, kwa sababu yamekosa malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama wanyama wanavyolia kwa huzuni! Makundi ya ng'ombe yanahangaika, kwa sababu yamekosa malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka. Neno: Bibilia Takatifu Jinsi gani ng’ombe wanavyolia! Makundi ya mifugo yanahangaika kwa sababu hawana malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka. Neno: Maandiko Matakatifu Jinsi gani ng’ombe wanavyolia! Makundi ya mifugo yanahangaika kwa sababu hawana malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka. BIBLIA KISWAHILI Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika. |
Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli waliokutanika kwake, walikuwako pamoja naye mbele ya sanduku, wakichinja sadaka kondoo na ng'ombe, wasioweza kuhesabiwa wala idadi yao kujulikana kwa kuwa wengi.
Hata lini itaomboleza nchi, na kukauka majani ya nchi yote? Kwa ajili ya mabaya yao wakaao ndani yake, wanyama wameangamia na ndege pia; kwa sababu walisema, Yu kipofu katika njia zetu.
Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.
Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe; Kwa maana vijito vya maji vimekauka, Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.
Naye alisema, BWANA atanguruma toka Sayuni, Atatoa sauti yake toka Yerusalemu; Na malisho ya wachungaji yatakauka, Na kilele cha Karmeli kitanyauka.
Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;
Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.
Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina uchungu pamoja hata sasa.