Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
Yeremia 48:3 - Swahili Revised Union Version Sauti ya kilio toka Horonaimu, Ya kutekwa na uharibifu mkuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikiliza! Kilio kutoka Horonaimu: ‘Maangamizi na uharibifu mkubwa!’ Biblia Habari Njema - BHND Sikiliza! Kilio kutoka Horonaimu: ‘Maangamizi na uharibifu mkubwa!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikiliza! Kilio kutoka Horonaimu: ‘Maangamizi na uharibifu mkubwa!’ Neno: Bibilia Takatifu Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. Neno: Maandiko Matakatifu Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. BIBLIA KISWAHILI Sauti ya kilio toka Horonaimu, Ya kutekwa na uharibifu mkuu. |
Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.
Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu.
Mtu huyo na awe kama miji ile, ambayo BWANA aliiangamiza, asijute; na asikie kilio asubuhi, na kelele za fujo adhuhuri;
BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.
Toka kilio cha Heshboni mpaka Eleale, naam, mpaka Yahasa, wametoa sauti zao, toka Soari mpaka Horonaimu, hata Eglath-shelishia; maana maji ya Nimrimu nayo yatakuwa ukiwa.
Kwa maana watu wapandapo huko Luhithi Watapanda wasiache kulia; Nao watu wateremkapo huko Horonaimu Wameisikia huzuni ya kilio cha uharibifu.