Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 47:2 - Swahili Revised Union Version

2 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini, nayo yatakuwa mto uliofurika; yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo, mji na wakazi na wanaoishi humo. Watu watalia, wakazi wote wa nchi wataomboleza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini, nayo yatakuwa mto uliofurika; yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo, mji na wakazi na wanaoishi humo. Watu watalia, wakazi wote wa nchi wataomboleza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini, nayo yatakuwa mto uliofurika; yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo, mji na wakazi na wanaoishi humo. Watu watalia, wakazi wote wa nchi wataomboleza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini, yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana. Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyo ndani yake, miji na wanaoishi ndani yake. Watu watapiga kelele; wote wanaoishi katika nchi wataomboleza

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Hili ndilo asemalo bwana: “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini, yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana. Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake, miji na wale waishio ndani yake. Watu watapiga kelele; wote waishio katika nchi wataomboleza

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.

Tazama sura Nakili




Yeremia 47:2
32 Marejeleo ya Msalaba  

Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Kama ningekuwa na njaa singekuambia, Maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.


Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo,


Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.


Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti enyi wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake.


Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.


Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya madari ya nyumba?


Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.


Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.


Ndipo BWANA akaniambia, Toka kaskazini mabaya yatatokea, na kuwapata watu wote wakaao katika nchi hii.


Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.


Neno hili ndilo ambalo BWANA alimwambia Yeremia, nabii, kueleza jinsi Nebukadneza, mfalme wa Babeli, atakavyokuja na kuipiga nchi ya Misri.


Misri ni mtamba mzuri sana, lakini uharibifu umekuja, Umekuja utokao pande za kaskazini.


Binti ya Misri ataaibishwa; Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.


Jinsi alivyovunjika! Ombolezeni! Jinsi Moabu alivyogeuza kisogo kwa haya! Hivyo ndivyo Moabu atakavyokuwa dhihaka, na sababu ya kuwashangaza watu wote wamzungukao.


BWANA asema hivi, Tazama, watu wanakuja, wakitoka katika nchi ya kaskazini; na taifa kubwa litaamshwa, litokalo katika pande za mwisho wa dunia.


Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.


Na wale wenye silaha mfano wa gharika watagharikishwa mbele yake, na kuvunjika, naam, mkuu wa maagano pia.


Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui zake hata gizani.


maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.


Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.


Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige mayowe kwa sababu ya mateso yenu yanayowajia.


Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;


Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo