Wakuu wa watu wamekusanyika, Kama watu wa Mungu wa Abrahamu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.
Waebrania 4:9 - Swahili Revised Union Version Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Basi, imebaki raha ya Sabato kwa ajili ya watu wa Mungu; Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo basi, imebaki raha ya Sabato kwa ajili ya watu wa Mungu; BIBLIA KISWAHILI Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu. |
Wakuu wa watu wamekusanyika, Kama watu wa Mungu wa Abrahamu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.
Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa makabila ya watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.
Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa muda;
Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika pumziko lake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.
Maana sisi tulioamini tunaingia katika pumziko lile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia pumzikoni mwangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.
ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.