Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Waebrania 4:13 - Swahili Revised Union Version Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu. Biblia Habari Njema - BHND Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu. Neno: Bibilia Takatifu Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye lazima tutawajibika kwake. Neno: Maandiko Matakatifu Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mwenyezi Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu. BIBLIA KISWAHILI Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake. |
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu);
Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.
Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na Injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee malipo ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, yawe ni mema au mabaya.
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.