Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Waebrania 10:13 - Swahili Revised Union Version tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema anangoja maadui zake wafanywe kama kibao chini ya miguu yake. Biblia Habari Njema - BHND anangoja maadui zake wafanywe kama kibao chini ya miguu yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza anangoja maadui zake wafanywe kama kibao chini ya miguu yake. Neno: Bibilia Takatifu Tangu wakati huo anangoja hadi adui zake wawekwe chini ya miguu yake, Neno: Maandiko Matakatifu Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake, BIBLIA KISWAHILI tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. |
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi katika mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?
Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wa kulia Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?