Waebrania 1:13 - Swahili Revised Union Version13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wa kulia Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema13 Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND13 Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza13 Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu13 Je, ni kwa malaika yupi Mungu aliwahi kusema, “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako”? Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu13 Je, ni kwa malaika yupi ambaye Mwenyezi Mungu amepata kumwambia wakati wowote, “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako”? Tazama suraBIBLIA KISWAHILI13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wa kulia Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Tazama sura |
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.