Na mimi nikatuma wajumbe kwao, nikasema, Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, siwezi kushuka, kwa nini niwashukie na hapo kazi isimame?
Nehemia 6:4 - Swahili Revised Union Version Nao wakaniletea mwito huo mara nne; nikawajibu maneno yale yale. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waliendelea kunitaka niende kwao mara nne, lakini nikawapa jibu lilelile. Biblia Habari Njema - BHND Waliendelea kunitaka niende kwao mara nne, lakini nikawapa jibu lilelile. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waliendelea kunitaka niende kwao mara nne, lakini nikawapa jibu lilelile. Neno: Bibilia Takatifu Walinitumia ujumbe huo huo mara nne, na kila mara nikawapa jibu lile lile. Neno: Maandiko Matakatifu Mara nne walinitumia ujumbe wa namna iyo hiyo, na kila mara niliwapa jibu lile lile. BIBLIA KISWAHILI Nao wakaniletea mwito huo mara nne; nikawajibu maneno yale yale. |
Na mimi nikatuma wajumbe kwao, nikasema, Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, siwezi kushuka, kwa nini niwashukie na hapo kazi isimame?
Ndipo Sanbalati akamtuma kwangu mtumishi wake vile vile mara ya tano, na barua wazi mkononi mwake;
lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
ambao hata saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi.
Delila akamwambia Samsoni, Tazama, umenidhihaki, na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, waweza kufungwa kwa kitu gani?
Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali niambie asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe.