tena katika kabila la Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu.
Nehemia 12:29 - Swahili Revised Union Version tena kutoka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema pia kutoka Beth-gilgali, eneo la Geba na Azmawethi, kwa sababu waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kandokando ya Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND pia kutoka Beth-gilgali, eneo la Geba na Azmawethi, kwa sababu waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kandokando ya Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza pia kutoka Beth-gilgali, eneo la Geba na Azmawethi, kwa sababu waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kandokando ya Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu kutoka Beth-Gilgali, na kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu kutoka Beth-Gilgali, na kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI tena kutoka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu. |
tena katika kabila la Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu.
Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Betheli na vijiji vyake;
Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi;
Tena nikagundua kwamba Walawi hawakupewa sehemu zao; Hivyo Walawi na waimbaji walioongoza ibada, kila mtu amerudi shambani mwake.
Je! Haiwi ng'ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waishio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More?
Tena katika kabila la Benyamini, Gibeoni pamoja na mbuga zake za malisho, na Geba pamoja na mbuga zake za malisho;
BWANA akamwambia Yoshua, Siku hii ya leo nimeivingirisha hiyo aibu ya Misri iondoke juu yenu. Kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Gilgali, hata hivi leo.