Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Nehemia 11:31 - Swahili Revised Union Version Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Betheli na vijiji vyake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa kabila la Benyamini walikaa Geba, Mikmashi, Ai, Betheli na vijiji vinavyoizunguka. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa kabila la Benyamini walikaa Geba, Mikmashi, Ai, Betheli na vijiji vinavyoizunguka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa kabila la Benyamini walikaa Geba, Mikmashi, Ai, Betheli na vijiji vinavyoizunguka. Neno: Bibilia Takatifu Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake, Neno: Maandiko Matakatifu Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake, BIBLIA KISWAHILI Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Betheli na vijiji vyake; |
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakakaa toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
tena kutoka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu.
Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini.
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hadi hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.
Samweli akasema, Umefanya nini? Naye Sauli akasema, Ni kwa sababu niliona ya kuwa watu wanatawanyika mbali nami, na wewe hukuja siku zile zilizonenwa; nao Wafilisti wamekusanyika pamoja huko Mikmashi;
Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake.