Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arubaini; nayo maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi.
Mwanzo 7:12 - Swahili Revised Union Version Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arubaini mchana na usiku. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mvua ikanyesha nchini siku arubaini mchana na usiku. Biblia Habari Njema - BHND Mvua ikanyesha nchini siku arubaini mchana na usiku. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mvua ikanyesha nchini siku arubaini mchana na usiku. Neno: Bibilia Takatifu Mvua ikanyesha juu ya dunia siku arobaini usiku na mchana. Neno: Maandiko Matakatifu Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana. BIBLIA KISWAHILI Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku. |
Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arubaini; nayo maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi.
Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arubaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;
Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arubaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arubaini, mchana na usiku.
Nikakaa mle mlimani kama hapo kwanza, siku arubaini usiku na mchana; BWANA akanisikiza wakati huo nao; BWANA asitake kukuangamiza.
Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.
Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano BWANA alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.