Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli.
Mwanzo 21:5 - Swahili Revised Union Version Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka mia moja, alipozaliwa mwana wake Isaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 100 wakati mwanawe Isaka alipozaliwa. Biblia Habari Njema - BHND Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 100 wakati mwanawe Isaka alipozaliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 100 wakati mwanawe Isaka alipozaliwa. Neno: Bibilia Takatifu Ibrahimu alikuwa na umri wa miaka mia moja Isaka mwanawe alipozaliwa. Neno: Maandiko Matakatifu Ibrahimu alikuwa na miaka 100 wakati Isaka mwanawe alipozaliwa. BIBLIA KISWAHILI Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka mia moja, alipozaliwa mwana wake Isaka. |
Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli.
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Naye Abrahamu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa nyama ya govi lake.
Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.
Na alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari, akisema, Umezaliwa mtoto wa kiume; na kumfurahisha sana.
Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia moja), na hali ya utasa wa tumbo lake Sara.