akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Mwanzo 18:4 - Swahili Revised Union Version Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtaletewa maji kidogo ili mnawe miguu na kupumzika chini ya mti. Biblia Habari Njema - BHND Mtaletewa maji kidogo ili mnawe miguu na kupumzika chini ya mti. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtaletewa maji kidogo ili mnawe miguu na kupumzika chini ya mti. Neno: Bibilia Takatifu Acha yaletwe maji kidogo, nanyi mnawe miguu yenu, na mpumzike chini ya mti huu. Neno: Maandiko Matakatifu Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. BIBLIA KISWAHILI Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. |
akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
Na mtu yule akaingia katika nyumba, akawafungua ngamia; naye akatoa majani na malisho kwa ngamia, na maji ya kuoshea miguu yake, na miguu ya watu waliokuwa pamoja naye.
Mtu yule akawaleta wale watu nyumbani mwa Yusufu, akawapa maji, wakanawa miguu, akawapa punda wao chakula.
Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.
na awe ameshuhudiwa kwa matendo mema; katika kulea watoto, kuwa mkaribishaji, kuwaosha watakatifu miguu, kuwasaidia wateswao, na kujitolea kutenda wema katika hali zote.
Basi akamkaribisha ndani ya nyumba yake, akawapa punda chakula; nao wakaosha miguu, wakala na kunywa.
Naye akainuka na kujiinamisha kifudifudi mpaka chini, akasema, Tazama, mjakazi wako ni mtumishi wa kuwaosha miguu watumishi wa bwana wangu.