Mwanzo 10:15 - Swahili Revised Union Version Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kanaani alikuwa babu yake Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Biblia Habari Njema - BHND Kanaani alikuwa babu yake Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kanaani alikuwa babu yake Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Neno: Bibilia Takatifu Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, Neno: Maandiko Matakatifu Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, BIBLIA KISWAHILI Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, |
nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;
Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
Naye Daudi akatuma mtu akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
kisha wakaja Gileadi, na nchi ya Wahiti huko Kadeshi; kisha wakaja Dani, na kutoka Dani wakazunguka mpaka Sidoni,
nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona uchungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali.
kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
Wakaao Sidoni na Arvadi ndio waliovuta makasia yako; wana wako wenye akili, Ee Tiro, walikuwa ndani yako, ndio waliokuwa rubani zako.
BWANA akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza mpaka kufikia Sidoni ulio mkuu, tena hadi kufika Misrefoth-maimu, tena hata kufikia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawaua wote, wasibakize hata mtu mmoja
Ndipo Daudi akajibu, akamwambia Ahimeleki, Mhiti, na Abishai, mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, akisema, Ni nani atakayeshuka pamoja nami kwa Sauli kambini? Abishai akasema, Mimi nitashuka pamoja nawe.