Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Methali 8:8 - Swahili Revised Union Version Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kinywa changu kitatamka maneno ya kweli, udanganyifu ni haramu midomoni mwangu. Biblia Habari Njema - BHND Kinywa changu kitatamka maneno ya kweli, udanganyifu ni haramu midomoni mwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kinywa changu kitatamka maneno ya kweli, udanganyifu ni haramu midomoni mwangu. Neno: Bibilia Takatifu Maneno yote ya kinywa changu ni ya haki; hakuna mojawapo lililopotoka au la ukaidi. Neno: Maandiko Matakatifu Maneno yote ya kinywa changu ni haki; hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi. BIBLIA KISWAHILI Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. |
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,