Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 8:28 - Swahili Revised Union Version

Alipofanya imara mawingu yaliyo juu; Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

wakati alipoimarisha mawingu mbinguni, alipozifanya imara chemchemi za bahari;

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

wakati alipoimarisha mawingu mbinguni, alipozifanya imara chemchemi za bahari;

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

wakati alipoimarisha mawingu mbinguni, alipozifanya imara chemchemi za bahari;

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

wakati aliweka mawingu juu na kuziweka imara chemchemi za bahari,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

wakati aliweka mawingu juu na kuziweka imara chemchemi za bahari,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Alipofanya imara mawingu yaliyo juu; Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 8:28
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.


Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.


Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.


chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;


Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake.


Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?


Kwa kukemea kwako yakakimbia, Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi,


Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele,


Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;


Alipozithibitisha mbingu nilikuwako; Alipopiga duara katika uso wa bahari;


Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;


Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.