Methali 8:18 - Swahili Revised Union Version Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utajiri na heshima viko kwangu, mali ya kudumu na fanaka. Biblia Habari Njema - BHND Utajiri na heshima viko kwangu, mali ya kudumu na fanaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utajiri na heshima viko kwangu, mali ya kudumu na fanaka. Neno: Bibilia Takatifu Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri unaodumu na mafanikio. Neno: Maandiko Matakatifu Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri udumuo na mafanikio. BIBLIA KISWAHILI Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. |
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang'anywa.
Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu.
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.