Methali 7:2 - Swahili Revised Union Version Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Biblia Habari Njema - BHND Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Neno: Bibilia Takatifu Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Neno: Maandiko Matakatifu Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. BIBLIA KISWAHILI Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. |
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
Lakini Yeremia akasema, La! Hawatakutoa. Nakusihi, uitii sauti ya BWANA katika hayo ninayokuambia; ndivyo itakavyokufaa, na nafsi yako utaishi.
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.
Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho;
Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.