huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.
Methali 7:13 - Swahili Revised Union Version Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu, na kwa maneno matamu, akamwambia: Biblia Habari Njema - BHND Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu, na kwa maneno matamu, akamwambia: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu, na kwa maneno matamu, akamwambia: Neno: Bibilia Takatifu Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia: Neno: Maandiko Matakatifu Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia: BIBLIA KISWAHILI Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, |
huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.
Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.
Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Watu huwapa makahaba wote zawadi, bali wewe unawapa wapenzi wako wote zawadi zako, na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote, kwa ajili ya mambo yako ya kikahaba.
Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi.
Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie BWANA dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hiyo pigo lilikuwa katika mkutano wa BWANA.
Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.