Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.
Methali 6:33 - Swahili Revised Union Version Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atapata majeraha na madharau; fedheha atakayopata haitamtoka. Biblia Habari Njema - BHND Atapata majeraha na madharau; fedheha atakayopata haitamtoka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atapata majeraha na madharau; fedheha atakayopata haitamtoka. Neno: Bibilia Takatifu Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe; Neno: Maandiko Matakatifu Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe; BIBLIA KISWAHILI Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. |
Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.
kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa kuhusu Uria, Mhiti.
Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.