Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 1:6 - Swahili Revised Union Version

6 Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa Bath-Sheba mke wa Uria).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa Bath-Sheba mke wa Uria).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa Bath-Sheba mke wa Uria).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Yese akamzaa Daudi, aliyekuwa mfalme. Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme. Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;

Tazama sura Nakili




Mathayo 1:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Daudi akatuma mtu akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?


Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo, Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;


na Uria, Mhiti; idadi yao ilikuwa watu thelathini na saba.


kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa kuhusu Uria, Mhiti.


Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai;


Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani;


na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;


tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.


Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;


Maombi ya Daudi mwana wa Yese, yamekwisha.


Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.


Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;


Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;


na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa Daudi.


BWANA akamwambia Samweli, utamlilia Sauli hadi lini, kwa kuwa mimi nimemkataa asiwatawale Waisraeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakutuma kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.


Basi Daudi alikuwa mwana wa yule Mwefrata, wa Bethlehemu ya Yuda, aliyeitwa jina lake Yese; naye huyo alikuwa na wana wanane; na yeye mwenyewe alikuwa mzee siku za Sauli, na mkongwe miongoni mwa watu.


Basi Sauli akamwuliza, Wewe, kijana, u mwana wa nani? Naye Daudi akamjibu, Mimi ni mwana wa mtumishi wako, Yese, mtu wa Bethlehemu.


hata ninyi nyote mkanifitinia, wala hapana mtu anifunuliaye habari hii mwanangu afanyapo agano na mwana wa Yese, wala hapana mmoja wenu anayenisikitikia, wala kunifunulia ya kuwa mwanangu amemchochea mtumishi wangu, anivizie kama hivi leo?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo